http://www.kbc.co.ke/story.asp?id=15555&categoryid=5
KBC
Taifa

Kibaki ashauriana na Aga Khan

Web posted on:Monday, February 17, 2003
By PPS

Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa Waislamu wa jamii ya Ismailia msitahiki Aga Khan wamefanya mashauri ya muda mrefu katika Ikulu ya Nairobi.

Waliokuweko wakati wa mashauri hayo ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Bwana Kalonzo Musyoka, katibu katika wizara hiyo Peter ole Nkuraiya na mkuu wa itifaki Bwana George Owuor.

Shirika la maendeleo la Aga Khan limekuwa likihusika na miradi mingi hapa nchini kwa miongo kadhaa ambako wakfu wa Aga Khan umekuwa ukufadhili mipango ya elimu, afya na ustawi wa sehemu za mashambani.

Kitengo cha elimu cha Aga Khan huendesha shule kumi na tano kote nchini ilihali kitengo cha huduma za afya husimamia hospitali tatu kuu katika miji ya Nairobi, Kisumu na Mombasa.

Wakfu wa Aga Khan pia umekamilisha mipango ya kutoa mafunzo ya shahada ya digrii kwa wauguzi haoa nchini.

Hazina ya Aga Khan ya ustawishaji uchumi pia huimarisha biashara na ustawi wa sekta ya kibinafsi katika nyanja mbali mbali kama vile viwanda vya utayarishaji bidhaa za kilimo, upakiaji wa bidhaa na utaoji wa kawi.

Hazina hiyo pia husimamia mahoteli ya Serena na taasisi za fedha kama vile Diamond trust Bank na Jubilee Insurance Company.